Total Pageviews


Breaking News

Saturday, January 31, 2015

Je,Man United italipiza kichapo cha 5-3?

Mechi kati ya Leicester na Man United ambapo Leicester ilipata ushindi wa 5-3
Huku Manchester United ikitarajiwa kuchuana na Leicester katika uwanja wa nyumbani wa Old Trafford,kiungo wa kati wa Manchester United Michael Carrick hatoshiriki katika mechi yoyote kwa kipindi cha wiki tatu baada ya kupata jeraha la misuli.
Ashley Young anakaribia kupona jeraha baada ya kuumia nyuma ya goti lake,huku Jonny Evans na Chris Smalling wakitarajiwa kushiriki.

Mathew Upson huenda akarejea tena katika kikosi cha kwanza cha Leicester baada ya kupona jereha la goti alilopata kabla ya msimu kuanza.
Matty James anahudumia marufuku,Riyad Mahrez bado yuko Afrika akiichezea timu ya taifa lake ya Algeria huku Kasper Schmeichel na Chris Wood wakiwa bado wako nje na majeraha.

No comments:

Post a Comment

Designed By MR.PRIME 2015