Huku Manchester United ikitarajiwa kuchuana na Leicester katika uwanja wa nyumbani wa Old Trafford,kiungo wa kati wa Manchester United Michael Carrick hatoshiriki katika mechi yoyote kwa kipindi cha wiki tatu baada ya kupata jeraha la misuli.
Ashley Young anakaribia kupona jeraha baada ya kuumia nyuma ya goti lake,huku Jonny Evans na Chris Smalling wakitarajiwa kushiriki.