Total Pageviews


Breaking News

Friday, January 30, 2015

Mashabiki wamzawadia gari msuva


Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, kwa miezi kadhaa sasa amekuwa akimiliki gari aina ya Toyota Altezza, sasa imebainika kuwa kumbe alipata gari hilo kutoka kwa mashabiki wa timu yake na siyo viongozi wa Yanga.

Msuva ambaye amekuwa kwenye kiwango kizuri katika siku za hivi karibuni kiasi cha kujihakikishia namba kwenye kikosi cha Yanga, amefunguka jinsi alivyopata gari hilo na kuongeza kuwa amewazawadia wazazi wake nyumba kutokana na uwepo wake katika mchezo wa soka.
Kiungo huyo wa zamani wa Azam ya watoto na Moro United, amefunguka kuwa kabla ya kuingia katika soka, alikuwa dansa wa muziki lakini mchezo huo umempa mafanikio makubwa ikiwemo gari, nyumba na mshahara mzuri.

No comments:

Post a Comment

Designed By MR.PRIME 2015