Total Pageviews


Breaking News

Thursday, January 29, 2015

Mtoto wa miaka 8 ahojiwa kuhusu ugaidi


Ufaransa imegubikwa na hofu baada ya mashambulizi ya Januari 8 dhidi ya jarida la Charlie Hebdo

Mtoto mwenye umri wa miaka 8 alihojiwa na polisi nchini Ufaransa kwa nusu saa Jumatano baada ya madai kwamba alitoa matamshi ya kuwasifu magaidi akiwa shuleni.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la AP, mtoto huyo alikataa kuungana na wenzake darasani kwa kimya cha dakika moja kuwakumbuka watu 12 waliouawa na wanaume wawili waliokuwa wamejihami mjini Paris Ufaransa mapema mwezi huu.

Shambulizi lilitokea katika ofisi za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo Januari tarehe saba kufuatia hatua ya jarida hilo kuchapisha picha za kumkejeli mtume Mohammad wa dini ya kiisilamu.
Wahariri wakuu wa jarida hilo pamoja na wafanyakazi wenginge waliuawa.
Mwalimu wa mtoto huyo alisema kuwa hakukataa tu kuungana na wenzake kwa kimya cha dakika moja bali pia aliwasifu washambuluaji.
Na kwa sababu ya hali ya usalama ilivyo nchini Ufaransa kwa sasa, mwalimu mkuu aliamua kumripoti mtoto huyo kwa polisi. Hata hivyo afisaa mmoja alisisitiza kwamba hakuna malalamiko yaliwasilishwa dhidi ya mtoto huyo.
"tulimwita mtoto huyo na babake kujaribu kuelewa ni vipi mtoto mwenye umri wa miaka 8 ana mawazo ya itikadi kali hivyo,'' alisema Marcel Authier afisaa mkuu wa mawasiliano katika eneo hilo.
"bila shaka mtoto huyu haelewi anachosema lakini ni muhimu kwetu kuhoji mawazo kama haya'' alisema Marcel.
Wakili wa mtoto huyo, Sefen Guez Guez, hakuweza kupatikana kwa maoni yake lakini kwenye akauti yake ya Tiwtter alisema kuwa mtoto huyo alikiri kusema: ''Ninawaunga mkono magaidi''.
Wakati polisi walipomhoji maana ya ''ugaidi'' mtoto huyo alisema '' sijui''
" Baba huyo na mtoto wake walishangazwa na namna walivyohojiwa, hali inayoonyesha wazi wasiwasi ambao umekumba Ufaransa tangu mashambulizi yaliyofanywa mapema mwezi huu'' ilisema taarifa ya shirika linalopambana na hofu dhidi ya waisilamu.

No comments:

Post a Comment

Designed By MR.PRIME 2015